Wamiliki wa mabasi mkoani Mwanza, wamesema kwamba
wameingiwa na hofu ya usalama wa maisha yao baada ya mwenzao
Samson Josia kupotea katika mazingira ya kutatanisha na baadaye
mwili wake kukutwa ukiwa umefungwa kwenye viroba na kutupwa
ndani ya Mto Mandaka.
Akizungumza jana kwa niaba ya wenzake wakati wa ibada ya mazishi ya
mmiliki huyo mabasi ya Super Sammy iliyofanyika nyumbani kwa
marehemu Mtaa wa Majengo Mapya mjini Magu, mmiliki wa mabasi ya
Msukuma, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ alisema tukio hilo limewafanya
wajihisi kuwa yeyote miongoni mwao anaweza kufuata kutekwa na
kuuawa.
Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike kuwabaini na kuwatia mbaroni
waliohusika,” alisema Msukuma ambaye pia ni mbunge wa Geita Vijijini
Akitoa salamu za Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa),
Ofisa Habari wa chama hicho, Mustapher Mwalongo licha ya kukabidhi
ubani wa Sh3 milioni kwa familia ya marehemu, alisema Taboa
itashirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha wahusika wanakamatwa
na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Pia, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Mapya, Renatus Ng’hula alisema
mauaji ya aina hiyo yanachafua haiba na taswira ya Taifa, “Tumekuwa
tukisoma na kuona matukio haya kupitia vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii; leo imefika kwetu kwa mtu tuliyemtegemea
kwenye masuala mengi ya kiuchumi na maendeleo.”
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mazishi,
kiongozi wa ukoo wa Mzuri, Yusufu Kijika alisema wauaji licha ya
kumchinja marehemu, pia walikata na kutenganisha na kiwiliwili miguu
yote miwili.
Alisema ingawa bado uchunguzi unaendelea, wanahusisha mauaji hayo
na madeni ambayo marehemu alikuwa akiwadai watu mbalimbali
walioshindwa kurejesha, “Tunahisi ukaribu na moyo wake wa kusaidia
wengine kupitia mikopo ndicho kimemponza; marehemu alikuwa
hadaiwi na mtu, bali yeye ndiye alikuwa akiwadai aliowakopesha.”
Alisema saa chache kabla ya kutoweka, Samson alimpigia simu mmoja
wa wake zake, Stumai Magembe akimwagiza kuandaa chakula cha
kutosha na sehemu ya kulala wageni aliosema angefika nao kwenye mji
wake mwingine ulioko jijini Mwanza.
“Kwa mujibu wa Stumai, simu hiyo alipigiwa saa 3:45 usiku wa Februari
27; lakini baada ya simu hiyo, marehemu hakuonekana wala kupatikana
kwenye simu hadi mwili wake ulipokutwa Mto Ndabaka siku tano baada
ya gari lake kukutwa likiwa limeteketezwa kwa moto katika Hifadhi ya
Serengeti,” alisema
Alisema familia ilifanya jitihada na kubaini kuwa wakati anapiga simu
usiku huo, alikuwa eneo la Buzuruga jijini Mwanza na kwamba
mawasiliano ya mwisho yalionekana akiwa hifadhi ya Serengeti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed alisema jana kuwa
watu wanaoshikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio hilo imefikia watano
baada ya mwingine kuongezeka juzi jioni.
alifika nyumbani hapo siku ambayo Samson alipotea akimuulizia na
kuondoka bila kueleza alichokuwa akimtafutia licha ya kuulizwa.
Mwili wa mfanyabiashara huyo ulikutwa ndani ya mto siku tano baada
ya gari yake ndogo aina ya Toyota Land Cruiser kukutwa ikiwa imeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Baadaye mwili wake uliokotwa na wavuvi waliokuwa wakiendelea na
shughuli zao ndani ya mto huo Machi 14
