Mkuu wa Shule ajinyongea Ofisini kwake....Aacha Ujumbe Ukimtaja Mkurugenzi wa Halmashauri


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma 

MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter  Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake  mapema leo asubuhi.

Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule  hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi  ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya  kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana  chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape  wananfunzi.

Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na  mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule  na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango  hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini.

Mwalim Isaac amesema Mwalimu  aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni  hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii, na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),alifika nyumbani  kwake juzi akitokea Dodoma.

Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo  Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi  akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa  walimu."Nilimuona kabisa tukasalimiana, nikamuuliza kama anaweza kuwa na chaki, akaingia ofisini akanipatia boksi moja la chaki.Nikachukua na  kisha nikampelekea mwalim aliyehizihitaji, alikuwa kwenye hali nzuri tu, lakini baada ya muda ndo tukio hilo likatokea,"amesema Kajoro.

Akizungumza baada ya kufika shuleni hapo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua  sababu ikiwa marehemu aliacha ujumbe wowote au laa.Hatujajua sababu  lakini ni muhimu jamii ikajenga utamaduni wa kueleza matatizo ya ndani  yanayoyasibu.Hiyo inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuepusha  madhara kama haya,"amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma  Martin Otieno amesema baada ya kupekuliwa kwa mwili wa marehemu walikuta karatasi imeandikwa ujumbe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko  Lusubiro Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo