Mkuu wa Mkoa apingana na Sumatra

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole - Sendeka amewaruhusu madereva wa bajaji Mkoani Njombe ambao walisimamishwa kufanya shughuli zao katika barabara kuu ya Njombe - Songea na kuruhusu bajaji kuongezwa mpaka bajaji 100 kutoka 55 ambazo zilikuwepo

Sendeka ameruhusu kufanya kazi bajaji baada ya kusimamishwa na mamlaka ya usafirishaji wa Majini na Nchi kavu Sumatra ambapo walisimamishwa kwa mujibu wa sheria ya bajaji na pikipiki ya mwaka 2010.
Aidha Madereva hao wa bajaji  wamedai kuwa walipeleka katika vituo ambavyo wanadai kuwa havikuwa na maslahi kwao na kwa biashara yao na hakukuwa rafiki kimiundombinu.
Hata hivyo wamiliki wa bajaji Mjini Njombe wamesema kuwa kwa muda wa wiki moja hawajaingiza fedha yoyote na kusema serikali imefanya vyema kutoa maamuzi hayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo