Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukinzana kwa taarifa zao kukinzana ambapo Kambanda Bwire alisema Nondo alienda kuripoti kutekwa kwake na yeye kudai kuwa walimkata, Mambosasa amesema hayo ni masuala ya tafsiri tu na ndiyo maana Nondo alipelekwa kwake na polisi wa Iringa kwa kuwa alikuwa chini ya ulinzi.
Akizidi kuwafafanulia wanahabari, Kamanda Mambosasa ameongeza kwamba yeye hakwenda kumchukua Nondo Polisi, lakini cha ajabu ni Nondo alipelekwa kwake na polisi na kuongeza kwamba ni ajabu kama alipewa uhuru halafu akawa huru kisha akapelekwa kituoni kwake bali hizo ni tafsiri za kukamatwa ambapo ameongeza "Unaponyimwa uhuru unakuwa upo chini ya ulinzi".
Pamoja na hayo Kamanda huyo ameongeza kwamba kitendo cha Nondo kutopelekwa mahakamani mpaka leo ni wanasubiria uchunguzi kukamilika kwani hata wao hawana 'interest za kukaa na mtu pasipo sababu.
Mbali na hato Kamanda Mambosasa amesema kwamba wanao ushahisi wa kutosha kwani mwanamke aliyekuwa akiwasiliana Nondo ameshapatikana na kuhojiwa na utafikishwa mahakamani.
Mambosasa pia ameweka wazi kwamba Nondo anashikiliwa kwa kosa alilolitenda la kudai kuwa ametekwa lakini pia ameshikiliwa kwa sababu za kiupelelezi.