Jakaya Kikwete atoa kauli juu ya polisi Tanzania

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kulipongeza jeshi la polisi Tanzania kwa kuweza kufanikisha kukamatwa kwa watu ambao walikuwa wakitumia vibaya majina yake, mkewe na mtoto wake kuwaibia watanzania

Yakiwa yamepita masaa kadhaaa toka Jeshi la Polisi nchina Tanzania litangaze kuwakamata wanawake watatu ambao walikuwa wakitumia majina ya Rais mstaafu na mkewe kwa kuiba fedha za wananchi kwa kuwalaghai kuwa wanatoa mikopo kupitia Vicoba kwa njia ya mtandao wa facebook, Kikwete aibuka na kumpongeza IGP Sirro. 
"Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa" alisema Jakaya Kikwete 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo