Nassari amezungumza hayo leo katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Arusha (RCC) ameeleza kuwa wananchi hasa maeneo ya Kisimiri hawajui kilimo kingine cha biashara zaidi ya bangi.
"Magunia mengi ya bangi yamekamatwa katika jimbo langu, lakini tulikubaliana kikao kilichopita cha RCC wananchi watafute zao mbadala walime hasa Pareto lakini hadi sasa hawajafundishwa kulima,”amesema.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa Arusha, Iddi Kimanta amemtaka Nassari kuwa mvumilivu kwani kulima bangi ni kosa na wala Serikali haitawavumilia ambapo amesema bodi ya Pareto imeahidi kuanzia Machi itaanza kutoa elimu.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe amemtaka Nassari kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufikia uamuzi kuwatafutia zao mbadala wananchi wa Meru kwani ingeweza kupiga marufuku kilimo cha bangi kama madawa ya kulevya mengine bila kutoa mbadala