Ridhiwani ametoa salamu hizo za pongezi kwa Mzee Kikwete na Mama Salma wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wake na wananchi wa Jimbo la Chalinze eneo la Kibindu.
"Maaara Paap. Mbunge wa Zamani/Mkulima kaibuka Mkutanoni.Tunamshukuru sana Mh. Raisi Mstaafu na Mama Salma Kikwete kwa mchango wao wa mifuko 300 ya Cement itakayofanikisha umaliziaji wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kwakonje na Nyumba ya walimu",amesema Ridhiwani.

Kwa upande mwingine, Mzee Kikwete tokea amalize muda wake wa kuongoza madarakani amekuwa akiendesha maisha yake kutumia kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo mbalimbali.
