Polisi agongwa na gari Dar es Salaam

Askari wa usalama barabarani anayejulikana kwa jina la Sajenti Peter amegongwa na gari leo asubuhi majira ya saa 5 wakati akitekeleza majukumu yake ya kusimamia usalama barabarani jijini Dar es Salaam

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa, ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara ya Kajenge na Rose Garden eneo la Sayansi ilipokuwa akiongoza magari
Juma Husein ambaye ni mkazi wa Sinza amesema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina Hucher maarufu kama Daladala kushindwa kufunga breki baada ya kusimamishwa na trafiki na kisha kuligonga gari dogo aina ya Subaru ambalo lilikuwa limeruhusiwa kuondoka na kusababisha ajali iliyopelekea trafiki huyo kugongwa na gari jingine. 
Ajali hiyo imetajwa kuhusisha magari matatu, majeruhi akiwemo trafiki huyo walikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi, aidha Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa trafiki huyo alivunjika mkono.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo