CHADEMA yafunguka kilichojiri wito wa Polisi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu Mkuu wake Dkt. Vicent Mashinji amefunguka na kudai wamehojiwa na Jeshi na Polisi kutokana na kosa la kufanya la mikusanyiko isiyokuwa ya halali wakati inafahamika walikuwa kwenye uchaguzi

Mashinji ameeleza hayo muda mchache alipotoka nje ya kituo cha Polisi 'Central' Jijini Dar es Salaam leo na kusema mpaka sasa kiongozi ambaye hajafika kituoni hapo kufanyiwa mahojiano ni Mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Freeman Mbowe ambae anafahamika kuwa ni mgonjwa.
"Kulikuwepo na mahojiano kuhusiana na masuala ya uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Kinondoni. Kama mnavyojua mimi sikuwepo siku ya kwanza lakini leo hii nimehojiwa kwa kosa la kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali wakati tunajua ilikuwa kipindi cha uchaguzi. Kwa upande wangu nimejaribu kuzungumza yote yaliyotokea na kikubwa kilichotaka kujulikana kutoka kwangu ni kwanini tulifanya maandamano", amesema Mashinji.
Pamoja na hayo, Mashinji ameendelea kwa kusema "kimsingi tulilazimika kwenda kuchukua barua zetu za utambulisho kwa ajili ya mawakala na tulikuwa ni viongozi pamoja na mawakala. Kwa hiyo hapakuwa na maandamano kama picha au taswira inayotakwa kujengwa kwa jamii, ilikuwa tu uzembe amabo ulifanyika kutoka katika Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuchelewa kuwapa mawakala wetu barua za kuwatambulisha katika vituo".
Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi limewataka viongozi hao kuripot tena kituoni hapo mnamo Machi 13 mwaka huu saa 1:00 asubuhi ili kuendelea na mahojiano mengine zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo