Akihitimisha operesheni maalum ya kitaifa ya kupambana na kudhibiti uvuvi na biasahara haramu ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa Ziwa Victoria iliyodumu kwa siku 40, katika ukumbi wa chuo cha benki kuu jijini Mwanza,Mh.Mpina amesema operesheni hiyo itaendelea hadi disemba mwaka huu ili kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa kabisa huku akidai hatasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kukwamisha juhudi za serikali.
Waziri Mpina pia ameonesha kuchukuzwa na kitendo cha askari wa wanyamapori wa hifadhi ya kisiwa cha Lubodo mkoani geita kuwazuia watendaji wa kikosi cha operesheni hiyo wakati wa msako dhidi ya uvuvi haramu.
Nje ya ukumbi wa kikao cha tathmini ya operesheni hiyo iliyopewa jina la operesheni sangara 2018 awamu ya kwanza, viongozi walioongoza operesheni hiyo wamedai kufanikiwa katika vita dhidi ya uvuvi haramu.
Operesheni hiyo ilianza Januari mosi mwaka huu,ambapo jumla ya wadau 1,200 waliopo kwenye sekta ya uvuvi nchini walikutwa na makosa mbalimbali na kutozwa faini ya shilingi Bilioni 4.7,huku tani 73 za samaki wasiokidhi kiwango wakigawiwa kwa wananchi,na tani 173 za mazao ya uvuvi zilitaifishwa,huku mali na zana mbalimbali za uvuvi zenye thamani kubwa ya fedha zikiteketezwa kwa moto.