Waziri awapongeza wananchi waliomfanyia Kitu Mbaya Muwekezaji

NAIBU waziri wa Madini,Stanslaus Nyongo amepongeza hatua ya wananchi zaidi ya 100,ambao ni wakazi wa kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu kufunga barabara ya kuingilia katika mgodi wa Nyarugusu Mine Co. limited na kuweka kambi eneo hilo usiku na mchana wakipika na kula,wakishinikiza walipwe fedha zao kama fidia ya mazao yao baada ya hekali zipatazo 273 kutiririshiwa maji yenye sumu kutoka katika mgodi huo.
Nyongo,aliye ziarani Mkoani Geita,ametoa pongezi hiyo muda mfupi baada ya kuwasili eneo hilo,ambapo kwa zaidi ya wiki moja sasa wananchi hao wameweka kambi,eneo hilo, kushinikiza uongozi wa Mgodi huo uwalipe fidia,huku akitishia kufuta reseni ya madini ya Mwekezaji huyo iwapo ataendelea na msimamo wa kutowalipa fidia wananchi hao
Awali wakiongea kwa jazba,mbele ya Naib Waziri huyo,wananchi hao wamedai kusikitishwa na hatua ya Mwekezaji huyo kugoma kuwalipa fidia kwa kisingizio cha tathimini ifanyike upya na wananchi wawe na hati miliki ya mashamba yao, ili hali wamekopa fedha zaidi ya million 20 zilizotumika kufungulia akaunti benki jambo ambalo linawaweka kwenye wakati mgumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo