Vifaranga hao walikamatwa katika eneo la mpakani mwa Kenya na Tanzania Namanga ambapo baada ya kukamatwa vifaranga wa kuku wa mayai 5000 wenye thamani ya Tsh 11,500,000 na Trei 416 zenye mayai, yenye thamani ya 3,120,000/ kwa pamoja viliteketezwa kwa moto kwa kuzingatia haki za wanyama (Animal welfare) ambapo kabla ya kuteketezwa mifugo hiyo ililazwa kwa kutumia dawa aina ya Farmaldehyde na kuhakikisha wamekufa kabla ya kuchomwa.
Mayai hayo pamoja na vifaranga vimekamatwa vikiingizwa nchini kinyume na sheria, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la chakula (FAO) ya mwezi Desemba ilitoa taadhari kuwa nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani Kenya na Uganda na nchi nyingine za Afrika ziko hatarini kuambukizwa mafua makali ya ndege.