Rais Dkt. John Magufuli amesema mara zote anaposikia matatizo yametokea eneo fulani fulani huwa anajiuliza akimbilie wapi ili aweze kupata msaada wa utatuzi wa jambo hilo bila ya kuleta athari yeyote katika taifa
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Februari 04, 2018) wakati alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam.
"Sisi viongozi wa serikali mara nyingi huwa tunawategemea viongozi wa makanisa na misikiti katika kutuongoza, nafahamu serikali haina dini lakini naheshimu sana dini na kuthamini mawaidha pamoja na mafundisho yanatolewa na viongozi wa dini wawe waislamu, wakristo hata wahindu tunayaheshimu sana", alisema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli aliendelea kwa kusema "siku zote sisi viongozi ndani ya serikali huwa tunafurahi sana kuona makanisa na misikiti ikiwa imetulia, unaposikia mahali fulani fulani kuna migogoro sisi viongozi na hasa mimi huwa najiuliza ninapopata matatizo ntakimbilia wapi. Kwa sababu makanisa na misikiti ni sehemu ya uponyaji wa roho zetu. Uponyaji wa roho ni mahali ambako kuna manufaa zaidi kuliko kwenye uponyaji wa mwili".
Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazambua jinsi taifa unaloliongoza roho zake zitakavyopotea.
Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo leo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt Jacob Chimeledya kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Willim Mkapa akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
aji Mkuu wa Tanzania Mstaafu Mhe Augustino Ramadhani akipiga kinanda kwenye sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama janeth Magufuli wakikomunika kwenye sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama janeth Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kushiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsihi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob Chimeledya kuketi kwenya kiti alichoandaliwa yeye wakati wa kupiga picha za pamoja wakati wa sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob Chimeledya na viongozi wengine wakati wa sherehe za kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
Picha na IKULU











