Prof. Jay azuiliwa kumuona Sugu

Mbunge Joseph Haule (Prof. Jay) akiwa ameambatana na mke wake Grace Haule wamezuiliwa na uongozi wa gereza la Ruanda liliopo mkoani Mbeya kumuona Bunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi "Sugu" pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga

Prof. Jay amethibitisha hayo kupitia moja ya kurasa zake za mtandao wa kijamii muda mchache alipowasili katika viwanja vya gereza la Ruanda kwa lengo la kutaka kuwajulia hali Sugu na Masonga ambao wamewekwa katika gereza hilo baada ya kunyimwa kwa dhamana katika kesi yao inayowakabiri.
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kosa la matumizi ya lugha ya fedhea dhidi ya Rais Dkt. Magufuli kesi yao itasikilizwa tena Februari 8 (Kesho) mwaka huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo