Kamanda Murilo amesema hayo leo Februari 24, 2018 wakati akiongea na moja ya chombo cha habari na kukanusha kuhusu taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa jeshi la polisi mpaka sasa halijawapeleka hospitali watuhumiwa hao licha ya kuwa na majeraha ya risasi.
"Moja ya kazi ya mtu anaitwa 'charge room officer' ni pamoja na kuangalia hali za watuhumiwa ambapo kila baada ya masaa manne anakagua mahabusu, anaangalia hali zao na wale ambao wapo kwenye hali ambayo inahitaji matibabu watu wanapelekwa hospitali na hiyo haitaji shinikizo ni haki ya kisheria ya mtuhumiwa ambayo sis tumeshaifanya kabla ya wao kuongea, sasa ni hospitali gani ni hospitali za serikali sasa kama kuna mtu anataka ampeleke kwenye hospitali yake hilo ni suala lingine, ila suala la kwenda hospitali ni suala la kawaida ambalo sisi hatuitaji mtuambie bali sisi tlishawapeleka hospitali kabla hata nyinyi hamjafikiria" alisema Murilo
Aidha Kamanda Murilo amedai kuwa jeshi la polisi litaendelea kukamata watu wengine kuhusiana na tukio hilo katika kuendelea kufanya uchunguzi na upelelezi kwani amedai kuwa tukio hilo lilihusisha kundi kubwa la watu hivyo wataendelea kuwakamata.
Jeshi la polisi Februari 16, 2018 inasemakan lilifyatua risasi za moto katika kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kuelekea kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni kudai barua za utambulisho wa mawakala wao, katika tukio hilo ndipo kilipotokea kifo cha binti Akwelina Akwilini ambaye alipigwa risasi ya kichwa na kupoteza maisha.
