Mwigulu na RPC wafanya uvamizi shambani


Waziri wa mambo ya ndani nchini,Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari  sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha


Mwigulu akishirikiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, (RPC)Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa zoezi hilo Mwigulu amesema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.
Aidha Waziri Mwigulu amewaambia askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo, Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini amewaambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani lakini inabidi waongeze juhudi pia katika kupambana na madawa ya kulevya yanayotengenezwa viwandani.
Niwapongeze sana songeni mbele na kazi ya kukamata madawa yote ya kulevya mmefanya kazi kubwa sana ya kukabiliana na madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani ongezeni bidii kukamata na yale yanayozalishwa viwandani,” Mwigulu
Naye Kamanda Mkumbo amesema kwamba jumla ya ekari sita za mashamba ya bangi zimeteketezwa na kusisitiza kwamba oparesheni hiyo ni endelevu katika mkoa wa Arusha na wilaya zake.
Walidhani kulima bangi katikati ya misitu hatutawakamata sisi tuna mbinu nyingi na hatutakubali kuona vijana wetu wanaharibikiwa kwasababu ya bangi”amesema Mkumbo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo