Muhimbili yafanya maajabu kwa watoto sita

Hospitali ya Taifa Muhimbili imewawashia vifaa vya usikivu watoto sita waliofanyiwa upasuaji maalumu wa kupandikiza vifaa vya usikivu, hatua ambayo leo hii imewawezesha watoto hao kwa mara ya kwanza kusikia sauti tangia wazaliwe

Daktari wa upasuaji Pua, Koo na Masikio Dkt. Edwin Liyombo, amesema kuwashwa kwa vifaa hivyo kunaifanya hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa na uwezo wa kufanya upasuaji wa kupandikisha vifaa vya usikivu, upasuaji ambao umekuwa unafanyika nje ya nchi tena kwa gharama kubwa.
Kwa upande wake, mwakilishi wa kampuni inayotengeneza vifaa hivyo ambaye pia ni daktari bingwa wa masuala ya sauti na upandikizaji vifaa vya usikuvu Dkt. Fayaz Jaffer, amesema itachukua takribani mwaka mmoja hadi watoto hao waweze kuzungumza ipasavyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo