Mbunge wa Njombe Mjini (CCM) Edward Mwalongo amesema takwimu zinazoonesha kuwa Mkoa wa Njombe Unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kitaifa, ni takwimu za kuonewa
"Hizi Takwimu za Njombe kuongoza kwa maambukizi mnazitoa wapi, ni za lini, au kuna kuonewa? kama mnataka takwimu halisi kwanini msifanye utafiti kila mwaka?" amesema
Ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja, ambapo amesema upo umuhimu wa takwimu kama hizo kuangaliwa upya
