Mbunge Nassari ashtakiwa kwa kesi ya shambulio

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kujibu shtaka la shambulio.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila mbele ya hakimu Jasmine Abdul amedai Desemba 14,2014 Nassari alimshambulia Neeman Ngudu.

Anadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Makiba kwa kumpiga mateke Ngudu na kumsababishia maumivu akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Muhalila amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na ameiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shtaka hilo.

Nassari anayetetewa na wakili Sheki Mfinanga alikana kutenda kosa hilo.

Hakimu Abdul aliahirisha kesi hadi Machi 6,2018 itakapotajwa.

Nassari alidhaminiwa na diwani Gabriel Mwanda wa Kata ya Ambuseri aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo