Makete: Wananchi wachachamaa, Fedha za Choo zanunulia Maparachichi

Diwani wa kata ya Ukwama Mh Augustino Tweve

Wananchi wa kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama wilayani Makete mkoani Njombe wamelaani vikali kitendo cha kamati ya kijiji hicho kutumia fedha za ujenzi wa choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Ihanga Kwa shughuli zingine tofauti hali iliyopelekea kusimama kwa ujenzi wa choo hicho.

Hayo yamejitokeza hii leo February 7, 2017 katika mkutano wa dharura wa kijiji cha Ihanga kilicholenga kujadili mambo mbali mbali likiwemo suala la sababu zilizopelekea kusimama kwa ujenzi wa choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Ihanga.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Ndelwa akisoma taarifa ya matumizi ya  fedha shilingi milioni tano ambazo zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi shuleni hapo, amesema kiasi cha fedha kimetumika katika shughuli mbali mbali za shule nje a Choo ikiwemo kununua miche ya parachichi ya kupanda shuleni hapo.

kufuatia maelezo hayo wananchi wa kijiji cha Ihanga hawakupendezwa na maelezo hayo kwa kuwa mipango ya pesa hizo ilikuwa kujengea choo cha wanafunzi shuleni, hivyo kusababisha malumbano makali mkutanoni hapo.

Kutokana na kujitokeza kwa hali ya kukosekana utulivu kwa wananchi kutokuwa na imani na suala hilo diwani wa kata ya Ukwama Agustino Tweve ametoa siku 7 kuanzia leo kwa kumuagiza mwenyekiti wa kamati ya shule kukaa na kamati yake ili waweze kulifuatilia suala hilo na waje na majibu ya kina ya kuwaeleza wananchi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Philipo Sanga amegoma kutekeleza maagizo ya Mh Diwani huku akidai hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake yuko tayari kuzipokea.

Mheshimiwa diwani Tweve baada ya kusikia kauli ya mwenyekiti wa kamamti ya shule Bw. Philipo Sanga kukaidi agizo lake amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo ataona utekelezaji wa agizo hilo ambalo linalalamikiwa na wananchi halitafanikiwa.



 Mwenyekiti wa kijiji akifafanua jambo

Choo hicho kilipofikia kwa sasa japo hakijakamilika ili kianze kutumika


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo