Basi la abiria lapinduka na kuua

Basi la abiria mali ya kampuni ya Tahmeed coach linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda nchini Kenya jijini Mombasa limepinduka JANA na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi watu wengine zaidi ya 20

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa basi hilo limepinduka katikati ya Msata na Kabuku mkoani katika eneo la Kitumbi Tanga na kudai kuwa mtu mmoja alifariki hapo hapo huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa.
"Ni kweli ajali imetokea imesababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 20, majeruhi wengine walipata majeraha madogo madogo hivyo tayari wamesharuhusiwa lakini majeruhi wengine watano nado wanapata matibabu" 
Hii ni ajali ya pili kwa mwaka huu inayohusisha basi za Tahmeed  kutokea katika eneo la Kitumbi, Januari 29, 2018 basi jingine liliwaka na kuteketea kwa moto katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo