Ajali hii ilivyoua watu na Kujeruhi wengine Kabuku Tanga

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kubwa kugongana na hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)  Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo imetokea saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Kabuku.

Alitaja mabasi hayo kuwa ni basi la kampuni ya AK Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar es salaam  lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE.

Alisema waliofariki ambao ni pamoja na Dereva wa hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.

ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukua majina yao kutokana na kuwasaidia kuwafikisha katika kituo cha afya Kabuku kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

Kaimu Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa chanzo cha ajali ni kutozingatiwa kwa sheria na alama za usalama barabarani kwa madereva hao.

Kamanda huyo wa Polisi alitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo