Watuhumiwa wa Uchawi wauawa kwa kupigwa Mawe

WANAUME wawili waliotuhumiwa kushiriki uchawi katika kaunti ndogo ya Igambang’ombe, kaunti ya Tharaka-Nithi kenya, Jumatano waliuawa kwa kupigwa mawe na umati wenye ghadhabu

Wawili hao, wenye umri wa miaka 55 na 60, walifurushwa kutoka nyumbani na kupelekwa katika soko la Kajuki ambapo waliuawa hadharani.
OCPD wa Chuka Igambang’ombe Bw Barasa Sayia aliambia vyombo vya habari kuwa, maafisa wa polisi waliarifiwa kuhusu kisa hicho lakini walipofika katika soko hilo, wanaume hao walikuwa washafariki kutokana na majeraha mabaya mwilini.
Mkuu huyo wa polisi alisema polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho ili kubaini wanakijiji waliohusika.
Bw Sayia aliwaonya wakazi dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao na kuwaomba kupiga ripoti kuhusu washukiwa kwa polisi ili sheria ifuate mkondo wake.
“Tumeanzisha uchunguzi wa kina ili kuwatia nguvuni na kuwashtaki wakazi waliohusika katika mauaji haya,” akasema Bw Sayia.
Wakazi waliohojiwa na Taifa Leo lakini wakaomba wasitajwe majina, walisema wanaume hao wawili wamekuwa wakiendesha shughuli za uchawi katika kijiji hicho kwa muda mrefu sana na walikuwa washukiwa wakuu wa vifo vingi ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa eneo hilo, hasa vya watoto.
“Wanakijiji walikuwa wamechoshwa na wazee hao kwa vitendo vyao dhalimu,” akasema mmoja wa mwanakijiji. Miili ya wawili hao ilipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Chuka kwa upasuaji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo