Waliowapa mimba wanafunzi kupimwa DNA

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magesa amesema suala la kuwapa mimba wanafunzi limekuwa na utata kwenye sheria, lakini sasa wamegundua njia mbadala ya kuwabaini wahusika wanaokatisha masomo ya wanafunzi

Akizungumza kwenye kikao kazi cha kukutana na watendaji wa serikali, Mhandisi Magesa amesema njia ya kisayansi ya kupima vinasaba itatumika kuwabaini baba wa watoto hao, na kuwachukulia hatua za kisheria.
'Watu wa DNA wanakuja hapa, tunasubiri tu wale watoto wajifungue halafu sisi tuthibitishe kwamba DNA yako na yule mtoto ni wewe”, amesema Mhandisi Magesa
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto amaefikia uamuzi huo baada ya kuwepo na taarifa za kuwepo kwa wanafunzi 159 waliopewa ujauzito na kukatisha masomo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo