Mkuu wa mkoa atumbua walimu zaidi ya 30

Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Alexander Mnyeti ametengua nafasi za wakuu wa shule za msingi zaidi ya 30 pamoja na maafisa elimu kata 13 wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kutokana na kuzembea kazini na kusababisha wilaya kushuka kitaaluma

Uamuzi huo ameutoa baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Tumaini Magesa kwenye kikao kazi cha kukutana na watendaji wa serikali, na kutoridhishwa na kiwango cha ufaulu, huku akumuonya afisa elimu wa shule za msingi na utumishi kushindwa kuwachukulia hatua watumishi
“Mkishindwa kusimamia walimu kufundisha tunawafuta, tunaweka wengine, ndani ya wiki mbili tatu nao tukiona wameshindwa tunafuta, na wenyewe tunaweka wengine hivyo hivyo mpaka mwisho, wakati huo tunawasubiri walimu wa sekondari na matokeo yao yakiwa ya hovyop nao tunafuta”, amesema Mnyeti.
Shule za wilaya hiyo zimeshindwa kufikia kiwango cha ufaulu wa wastani wa asilimia 50 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa mwaka 2017, na kitendo kilichomkera Mkuu wa Mkoa Mnyeti


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo