*UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA DSM (UVCCM DSM)*
Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dsm unalaani vikali Vitendo vilivyofanywa na Madiwani wa UKAWA kwa kuwafanyia Vurugu Madiwani wa CCM wa Jiji lakini pia na Mkurugenzi wa Jiji.
Vitendo hivi havikubaliki hata kidogo huu sasa umekuwa ndio mchezo wao *UKAWA* kulazimisha ushindi kwa hila.
*Ikumbukwe mwaka 2016 wakati wa uchaguzi wa kumpata Meya wa Jiji kulifanyika vurugu kama hizi na kusababisha kumdhalilisha RAS na kaimu Mkurugenzi wa Jiji kipindi kile na hatimaye RAS kufungua kesi dhidi ya udhalilishaji ule kwa Madiwani wa UKAWA*.
Aidha Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Dsm unalaani Vikali kitendo cha Diwani mmoja wa CCM kuupigia kura upinzani katika Uchaguzi wa *Naibu Meya wa Jiji uliofanyika jana Karimjee hall*, hali ya kwamba anajua kabisa *KURA* yake ilikuwa ni turufu ya ushindi au kulinda heshima ya Chama chetu , Huu ni *USALITI* mkubwa sana hakika tumeumia sana.
*Kwa Mujibu wa Katiba na Kanuni zote za CCM KOSA kubwa kuliko yote kwa Mwanachama wa CCM ni USALITI*.
Kwa taarifa za kiinterejensia Mfanyaji kosa ameshajulikana sioni sababu ya CCM ngazi husika kuchelea kufanya maamuzi ... Kitendo cha kuchelea kufanya maamuzi pia nalo ni kosa la kikao na wahusika wanaweza kuchukuliwa hatua, hivyo basi ni vyema hatua kali kwa Mujibu wa Vitabu vyetu vya CCM ikachukuliwa kwa *MSALITI* husika.
*Tuweke kumbukumbu sawa Mwaka jana kulikuwa na Uchaguzi kama huu wa Naibu Meya Manispaa ya Ilala ikatokea kama ya jana Diwani mmoja wa CCM bila ya haya akawapigia kura UKAWA, Tulilumbana wenyewe kwa wenyewe mwisho wa siku kukawa kimya hakuna aliyechukuliwa hatua na ndio maana Jana yamejirudia tena*.
Wakati unafanyika *Uchaguzi wa Naibu Meya Manispaa ya Ilala 2017 Uongozi wa Mkoa ulikuwa haujakamilika lakini kwa sasa naamini chini ya Mwenyekiti wetu Mama Kate Kamba, Wajina Komred Saady Kusilawe, Mwenezi Komred Simon Mwakifamba na Super MNEC Yusufu Majid maamuzi magumu na yenye tija kwa Chama chetu yatachukuliwa soon as possible*.
Vijana na Wanachama wa CCM wengi wameumia kwa tukio la jana yaani *CCM* tunawapa ushindi *UKAWA* ambao jana waliingia ukumbini wakijua wazi wanashindwa!!! Not serious hii si haki kwetu lazima adhabu kali ichukuliwe tena kwa haraka.
Mwisho tuwapongeze wale Madiwani wahadilifu waliopambana waziwazi kukitetea Chama tunajua walikuwa wanatimiza wajibu wao laki kiungwana lazima tuwape heshima ya *Pongezi wakiongozwa na Mstahiki Meya Chaurembo*.
UMOJA WA VIJANA SASA TUPO MACHO NA HATUPO TAYARI KUWACHEKEA WASALITI WASIPOWAADHIBU KWENYE CHAMA TUTAWAADHIBU SISI VIJANA MTAANI KAVUKAVU.
*CCM NDIO BABA CCM NDIO MAMA,,, MAPAMBANO YANAENDELEA*.
Kwa niaba ya Uongozi wa UVCCM Kanda Maalum Dsm.
By *SAADY KHIMJI Katibu wa Uhamsishaji na Chipukizi Mkoa wa Dsm*.UVCC