Waandishi wa habari nchini wameshauriwa kuandika habari zao kwa uhuru bila kuwa na woga wowote
Hayo yamesemwa jana na msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa idara ya habari maelezo DK Hassan Abasi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
Abbasi akijibu swali la mwandishi wa habari amesema tukio la kutekwa kwa mwandishi wa habari wa Mwananchi liachiwe yombo vya dola vilifanyie kazi kwa kuwa mpaka sasa haijajulikana kama ametekwa ama yuko wapi, lakini hilo lisiwakatishe tamaa waandishi wa habari katika kuandika habari zao za kweli
Amesema waandishi wa habari wakiandika habari za kweli serikali inazifanyia kazi mara moja akitolea mfano gazeti la jamhuri lililopongezwa na Rais Dkt John Magufuli kuandika habari ya mafuta bandarini na serikali ikachukua hatua na kuongeza kuwa hakuna haja ya wanahabari kujawa hofu katika kuandika habari zao