RC: Serikali yetu haipangiwi na Mtu

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amefunguka na kusema kuwa Serikali haiwezi kupangiwa wala watumishi wake hawawezi kupangiwa kazi za kufanya na Taasisi zisizo za kiserikali wala wafadhili

Zambi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji wa Zahanati na vituo vya afya mkoani humo ambapo amebaini kukithiri kwa uchafu katika Zahanati hizo huku ikisemekana moja ya Asasi isiyo ya Serikali imewazuia wahudumu wa afya kufanya usafi katika Zahanati kwa madai ya kuwa kazi ya kufanya usafi si jukumu lao na kuwataka wananchi ndiyo wafanye usafi huo.
"Naomba niseme tena kama Mkuu wa Mkoa GIZ ni wafadhili wetu tunawashukuru wanatusaidia lakini sasa wasituingilie kwenye utendaji wa kazi kwenye Zahanati zetu na vituo vya afya, mazingira yetu tunayajua sisi Zahanati iko hapa lakini mtu mwingine ana kaa kilomita mbili au tatu sasa unataka mtu huyo ndiyo aje afanye usafi halafu arudi nyumbani kwake akaendelee na majukumu mengine" alisema Zambi 
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Lindi amewataka wafadhili hao kutoingilia majukumu ya Serikali kwa kuwapangia watumishi wake namna ya kufanya kazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo