Polepole: Rais Magufuli hataongeza muda wa Kuwepo Madarakani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5-7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 13 wakati alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  IKulu, ndg. Humphrey Polepole na kumtuma awajulishe watanzania na wana CCM kwamba wapuuze mijadala hiyo kwani jambo hilo halijawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama.
Kupitia taarifa iliyotlewa na Ikulu, Rais Magufuli amemuagiza Polepole kuwajulisha watanzania na wana CCM kuwa wasikubali kuyumbishwa au kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2017.
Mjadala wa kuhusu kuongeza muda wa uongozi uliibuka pale Mbunge Kondoa Juma Nkamia alipoweka wazi hisia zake za kupeleka mjadala bungeni wa kutengeneza muswada utakaojadili viongozi wanaochaguliwa kukaa madarakani kwa miaka 7 badala ya mitano iliyopo sasa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo