Mwalimu adaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mlemavu

Mwalimu mmoja wa shule ya wanafunzi wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenye ulemavu na kumsababishia ujauzito

Akizungumza katika kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa na shirika la TCRS, Mkuu wa wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai, amesema kitendo kilichofanywa na mwalimu huyo sio cha kukifumbia macho huku mwanafunzi akiwa amekatisha kuendelea na masomo yake.
Mkuu huyo wa wilaya pia, akaeleza wilaya yake inavyoathirika na tatizo la tatizo la mimba za utotoni na utoro na kupelekea kufanya vibaya katika mitihani ya Kimkoa na Kitaifa.
Wilaya hiyo imeshika nafasi ya sita kati ya wilaya sita za mkoa wa Lindi katika matokeo ya mithani wa darasa la Saba mwaka jana, huku ikishika nafasi ya 160 Kitaifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo