Na Asha Shaban, Musoma
Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima ameufungua mgodi wa dhahabu wa Buhemba uliopo katika kijiji cha Magunga kata ya Mirwa wilayani Butiama baada ya kufungwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na kuwepo kwa mazingira mabaya ambayo yalipelekea wachimbaji zaidi ya sita kupoteza maisha
Vifo hivyo vilitokea baada ya wachimbaji hao wadogo kufukiwa na vifusi ndani ya mashimo ya dhahabu na baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika kuwa mgodi huo una mapungufu katika miundo mbinu na mashimo pamoja na kamba za kuingilia na kutoka shimoni ndipo ulifungwa hadi hapo utakapokidhi vigezo
Kufungwa kwa mgodi huo kulipelekea shughuli za uzalishaji mali kusimama katika mgodi huo hivyo kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu kwa wachimbaji hao pamoja na wananchi wanaozunguka mgodi huo .
mkuu wa mkoa alisema mgodi huo umefunguliwa ili vijana na wakazi wa eneo hilo wapate ajira kwani hakuna kazi nyingine yoyote wanayoifanya zaidi ya kutegemea mgodi huo.
Aliongezea kuwa usalama upo wa kutosha katika maeneo ya kazi na kwamba mgodi huo ni kwaajiri ya wakazi wa eneo hilo na hakuna mtu mwingine kutoka sehemu zingine kuja hapo kwaajiri ya shughuli hiyo.
Jumla ya mashimo 16 yamejengwa na kati yake 10 yamekidhi vigezo hivyo tayari kwa kuanza kazi na yote yamezungushiwa wigo na mkaguzi mkuu wa madini amejiridhisha na hatua hiyo hivyo kuruhusu kutumika
.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo aliwataka wachimbaji hao kuhakikisha wanalipa kodi inayotakiwa kwa serikali ili iweze kujipatia mapato kutokana na mgodi huo ambao
yatasaidia katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo elimu, afya na barabara
Alisema ili kuweza kunufaika kwa pamoja ni lazima uchimbaji uwe ni wenye kuleta tija kwani hakuwezi kuwa na tija kama hakuna uchimbaji wenye tija huku akiwataka wachimbaji hao kuzingatia na kufuata taratibu za kiusalama katika kazi zao.
Naibu waziri alitumia nafasi hiyo kuwaonya wale wenye tabia ya kutorosha madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani serikali haitaimfumbia macho yeyote atakaebainika kufanya hivyo kwani anashiriki kuikosesha serikali mapato.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi