Mbowe Asikitishwa Kesi ya Sugu Inavyoendeshwa

Mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe amedai amesikitishwa na namna inavyoendeshwa kesi ya Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga iliyoahirishwa leo.

Freeman Mbowe ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii leo katika viunga vya Mahakama ya mkoani Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuzitaka mamlaka husika zinazosimamia sheria nchini kujiangalia vizuri katika utendaji kazi wake.

"Tumesikitishwa kwa namba suala hili jinsi lilivyo shughulikiwa, sipendi kuingilia uhuru wa Mahakama, mienendo ya kimahakama lakini mimi kama raia na kiongozi nafikili vyombo vinavyostahili kutoa haki kwa wananchi vinawajibu wa kujiangalia vizuri. 

"Mahakimu, Majaji, Mawakili wa Serikali pamoja na Askari wenyewe hawa wote ni binadamu haina maana kwamba wao hawawezi kufanya makosa wao ni binadamu kama walivyo wengine", alisema Mbowe.

Kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga imehairishwa leo na kutajwa kusikilizwa Februari mbili baada ya Mawakili watatu kujitoa kuwasimamia katika kesi hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo