Manara: Hamjui navyoumia Simba kutupwa Nje

January 8 2018 wekundu wa Msimbazi Simba walirejea uwanjani kuwania nafasi yao ya kufuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2018 kwa kucheza dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A.
Simba walikuwa wanahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuitoa URA ya Uganda ambao wao walikuwa wanahitaji sare pekee ili wafuzu tofauti na Simba ambao walikuwa ni lazima washinde ili kama watataka kusonga mbele.
Bahati haikuwa ya Simba na dakika ya 48 URA wakapata goli la ushindi kupitia kwa Kalama Debossi na kuufanya mchezo umalizike kwa Simba kupoteza kwa goli 1-0 na kuyaaga mashindano hayo, baada ya game afisa habari wa Simba Haji Manara alitumia ukurasa wake wa instagram kuwaandikia wanasimba ujumbe huu.
“Kila sentesi niliyoandika nimefuta, hakuna neno linalotosha kuelezea hisia zangu kwa kilichotokea leo Amaan Stadium..nayajua maumivu ya wanasimba….shida yangu mimi ni msemaji kisha shabiki wa hii timu..najua sana pain yenu…but lazma maisha yasonge mbele…🙏🙏”>>>Manara


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo