Lowassa: Kumtajataja Mtulia Ni kumpa Kichwa wakati ni wa ovyo

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amefunguka na kuwataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa CCM Kinondoni Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa kichwa

Lowassa amesema hayo leo Januari 27, 2018 akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo leo maelfu ya wananchi wa Kinondoni wameweza kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA kwa hoja na sera mbalimbali kuelekea uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018. 
"Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu" alisema Lowassa 
Mbali na hilo Lowassa alimnadi Salum Mwalimu kwa kusema kuwa ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo