Zitto Kabwe amesema hayo leo Januari 31, 2018 wakati akichangia Bungeni juu ya mswada wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa watumishi wa sekta ya Umma na kuwataka wabunge kutoipitisha sheria hiyo kama Serikali haitaifanyia marekebisho kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha haki za kimsingi wanachana zaidi ya laki sita wa NSSF.
"Serikali inafanya marekebisho ya sheria ya NSSF, Sheria ya NSSF inatoa 'Health Insurance Benifit' kwa wanachama wa NSSF lakini sheria hii ambayo serikali inaileta hapa inaondoa 'Health Insurance Benefit' kwa wanachama wa NSSF hili ni jambo la hatari, sasa hivi NSSF wanazaidi ya wanachama laki sita kwa hiyo Serikali hii inakwenda kutunga sheria kuwaondoa watu laki sita kwenye takwa la kisheria la Health Insurance" alisema Zitto Kabwe
Mbali na hilo Zitto Kabwe aliweza kutoa ushauri ambao Serikali inaweza kuufuata ili mwisho wa siku wanachama wa NSSF waweze kupata haki yao ya msingi ya matibabu pindi mifuko hiyo itakapoonganishwa.
"Serikali inataka 'Health Insurance' zote ziwe zinatolewa na NHIF inaeleweka tunachopaswa kukifanya kwenye sheria ni kuweka provision inayosema kwamba fao hilo la Health Insuarance litatolewa na NHIF kwa NSSF kuchukua ile michango inayolipia Health Insurance na kuipeleka NHIF. Hivyo ukiwa na kadi ya NSSF na mwanachama wa NSSF moja kwa moja unakuwa wanachama wa NHIF, hii ndiyo njia bora kabisa ambayo Serikali inapaswa kufanya na nawashauru ndugu wabunge kama marekebisho haya hayatafanywa tusiipitishe sheria hii kwa sababu tunakwenda kuwaondoa watu laki sita kutoka kwenye 'Health Insurance'" alisisitiza Zitto Kabwe
