Hii ndio sababu polisi kukamata wajawazito

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Sebastian Waryuba , ametolea ufafanuzi suala lililoleta sintofahamu kwa jamii, la kuwakamata mabinti wanafunzi waliopata ujauzito na kuwapeleka polisi

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Waryuba amesema amefikia uamuzi wa kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia serikali kubaini watu waliosababisha kukatisha masomo kwa mabinti hao, ambao mara nyingi wamekuwa wakihofia kuwataja.
Mheshimiwa Waryuba amesema kuwa mabinti hao pamoja na wazazi wao wametoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali kwa kuwataja, huku wakionyesha kujutia baada ya kufikishwa polisi, lakini wote waliachwa huru baada ya kukamilisha mahojiano.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo