PICHA: Mtazame Hapa Kigogo wa CHADEMA Aliyejivua Uanachama na Kujiunga CCM Leo

Kiongozi mkubwa wa upinzani aliyejiunga na CCM leo ni Muslim Hassanali aliyekuwa mgombea ubunge Ilala kwa tiketi ya Chadema 2015 .

Pia alikuwa ni  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  na  mmoja kati ya watia saini wa ruzuku za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

 Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kujiunga CCM.

Tayari viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu tofautitofauti ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

Kiongozi huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo