Diwani wa CHADEMA Tarime ahamia CCM


Diwani wa kata ya Turwa  wilaya ya Tarime  mkoani Mara na mjumbe wa kamati kuu ya Wilaya Chadema Zakayo Chacha amebwaga manyanga na kukihama chama na kutimukia CCM.

Akizungumza  leo Januari 5,2018 na waandishi wa habari katika ukumbi wa Goldland Hotel Zakayo amesema kwa sasa haoni haja ya kuendelea kuwa kwenye chama ambacho hakuna dira.

Hata hivyo amewashukuru wananchi wake kumuunga mkono kipindi cha uongozi wake kwani umefanikiwa kupeleka maendeleo kwao ambayo ni tofauti na kipindi vingine vilivyopita huku akiwaomba kuendelea jumla ushirikiano katika kusukuma gurudumu mbele.
Na Waitara Meng’anyi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo