Dkt. Salim ameaga baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho. Waziri Mkuu huyo wa zamani amempongeza Mwenyekiti wa CCM Rais John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha Chama kuimarika.
Katika hatua nyingine Dkt. Salim amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake.
Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.