Uhamiaji wafunguka uchunguzi wa yule Askofu

Idara ya Uhamiaji nchini imesema sakata la kumuhoji uraia wake Askofu wa Jimbo la Ngara , Severine Niwemugizi, wataweka wazi pindi uchunguzi utakapokamilika

Hayo amesema leo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.
''Hizo ni taarifa za kiuchunguzi ambazo bado tunaendelea nazo, huwezi kuweka wazi kila kitu wakati bado tupo katika uchunguzi, tunapokuwa na shaka na mtu yoyote kuhusu uraia wake tunaruhusiwa kumuhoji,'' amesema Dr. Makakala.
Madai ya Askofu huyo kuhusu kuhoji upatikanaji wa katiba mpya ndio sababu ya kuhojiwa na idara hiyo, Dr. Anna amekanusha na kusema wawaache kwanza hadi uchunguzi utakapokamilika.
''Hayo ya kwake, naomba tusubiri uchunguzi hadi utakapo kamilika,'' ameongeza


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo