Ubakaji waongezeka nchini

Said Mwishehe,Blogu ya jamii

INASIKITISHA!Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Jeshi la Polisi nchini kusema kuwa mwaka huu wa 2017 matukio ya ubakaji na kunajisi watoto yameongezeka na kushika kasi ikilinganishwa na mwaka 2016

Imefahamika sababu ya kuongezeka kwa matukio hayo ni ushirikina, tamaa ya mwili na mmomonyoko wa maadili kwenye jamii ya Watanzania

Akizungumza Dar es Salaam leo, kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Boaz amefafanua makossa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka,kulawiti , wizi wa watoto, kutupa watoto, kunajisi na kusafirisha binadamu yameripotiwa

“Katika kundi hili makosa ambayo yameonekana kuongezeka ni makosa ya kubaka na kunajisi.Zipo sababu nyingi lakini kubwa ni ushirikina, kukosekana kwa maadili na tamaa ya mwili.

“Jeshi la Polisi tutaendelea kufuatilia wanaojihusisha na matukio hayo na kisha sharia ichukue mkondo wake.Tunaomba jamii nayo ishirikiane na jeshi lao kutoa taarifa dhidi ya wanaojihusisha na matukio ya aina hiyo,”amesema.

Ameongeza takwimu zinaonesha makosa ya kubaka na kunajisi yameongezeka. Novema mwaka 2016 makosa ya kubaka yaliyoripotiwa yalikuwa 6,985 ikilinganishwa na makosa 7,460 ambayo yameripotiwa mwaka huu.

Amesema hilo ni ongezeko la makosa 478 sawa na asilimia 6.8, wakati makosa ya kunajisi yalikuwa 16 kwa mwaka 2016 ikilinganishwa na makosa 25 mwaka huu wa 2017 na kufanya ongezeko la makosa 9 sawa na asilimia 56.3.

Kuhusu matukio ya wizi wa mali kwa kutumia silaha, unyang’anyi ,wizi wa pikipiki , wizi wa magari ,wizi wa mifugo na kuchoma moto nyumba. Amesema matukio ambayo yaliripotiwa mwaka 2016 yalikuwa makosa 34,830 wakati mwaka huu yameripotiwa makosa 29,677.Pungufu ni makosa 5,153.

Akizungumzia uhalifu wa fedha yanayohusu makosa ya noti bandia , wizi katika benki, wizi kwenye mashirika ya umma na makosa ya kughushi mwaka 2016, makosa yalikuwa 1,861 ikilinganishwa na makosa 1,526 yaliyoripotiwa kwa kipindi kama hicho mwaka huu.

Kuhusu ajali za barabarani, Boaz amesema ajali zilizotokea zimesababisha vifo vya watu 3,108 na majeruhi 8,898 kwa mwaka 2016 wakati mwaka huu watu waliokufa ni 2,491 na majeruhi ni 5,696.

“Uchunguzi wetu umebaini ajali nyingi zinasababishwa na vyanzo vikuu vitatu ambavyo zikiwamo za kibinadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri na sababu za kimazingira.“Sababu za kibinadamu ni pamoja na mwendo kasi,uzembe wa watembea kwa miguuu,”amesema.

Jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi au maeneo ya biashara.

“Tunaomba wananchi kutumia namba za simu za bure 111,112 na 0787 668306 ambayo hutumika na Jeshi la Polisi katika kupokea taarifa za uhalifu na wahalifu,”amesema Boaz.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo