Rais Magufuli atii agizo la Tume, Awasilisha fomu zake mapema

Rais John Magufuli amewasilisha fomu ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio wilayani Ilala jijini Dar es Salaam

Rais amewasilisha fomu hiyo leo Alhamisi Disemba 28, ikiwa ni siku moja baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwataka viongozi kuziwasilisha, ameipongeza sekretarieti kwa kazi inazofanya.
Pia, amemtaka Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo Desemba 31,2017.
“Ikifika Desemba 31, ambayo ni siku ya mwisho kwa mujibu wa sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema,” Magufuli 
Jaji mstaafu Nsekela amemshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo. Amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma si ombi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo