DCI Boaz amesema hayo leo Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.
"Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika" alisema DCI Boaz
Mbali hilo DCI aligusia kuhusu shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kusema kuwa jeshi la polisi linachukulia tukio hilo la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma 'serious'
"Jeshi la polisi linachukulia tukio hilo 'Serious' na sisi hatuwezi kujibishana na watu kwenye magazeti tunachukua hatua zote ambazo zinatuwezesha kutambua nani alitenda tukio hilo"alisema DCI Boaz.