Kasesela alisema hayo baada ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kusema baaadhi ya viongozi wao hata yeye wamekuwa wakipigiwa simu na kupewa ahadi nyingi nzuri ili waweze kuachia nafasi zao na kujiunga na CCM. Kufuatia kauli hiyo ya Lema ndipo hapo Mkuu wa Wilaya ya Iringa alipowataka CHADEMA wajiangalie kama wanasimamia misingi ya chama hicho.
"La msingi ni kumjenga mwanachama wako kiitikadi hasa kwa kumjengea imani. Kama hana imani na chama atahama tu kwani hayo uliyoyasema akibaki kwenye chama chake atayapata tu. La msingi kuangalia je wanachama wana imani?! Kubwa zaidi ni kujipima je, mnasimamia misingi ya chama?" alisema Kasesela