CHADEMA Mbeya wapata Pigo Kubwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mbeya kimepata pigo baada ya kumpoteza moja ya mwanachama wao na kiongozi, Jacob Kalua ambaye amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi amethibitisha hilo na kusema kuwa wao CHADEMA Mbeya na Kanda ya Nyanda za Juu (Nyasa) wamepoteza mtu muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho siasa za kibabe na mabavu zinahitajika. 
"Kamanda Jacob Kalua, ni pigo lingine kwa Mbeya na Kanda ya Nyanda za juu (Nyasa) kwa jumla. Tutaukosa ujasiri wako, hasa kipindi hiki cha siasa za kibabe na mabavu, kipindi ambacho makamanda wasio waoga kama wewe wanahitajika zaidi kwenye kazi ya ukombozi" alisema Joseph Mbilinyi
Mbali na Sugu pia Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche ameonyesha kusikitishwa na kifo cha kiongozi huyo na kusema kuwa alikuwa msaada mkubwa katika chama 
"CHADEMA imepoteza mpiganaji asiechoka nakumbuka nikiwa Mwenyekiti wa BAVICHA mara zote nilizokuja Mbeya ulivyonipokea, nakumbuka maandalizi yako ya mikutano, ulinzi na hata kuhakikisha tumekula vizuri. Tangulia mbele ya haki kaka ila umetuachia maumivu makubwa"ameandika John Heche 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo