Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete
mkoani Njombe Hii leo limetoa maamuzi dhidi ya mashauri mbalimbali ya kinidhamu
ya watumishi kadhaa ndani ya halmashauri hiyo
Mashauri hayo yamefikishwa kwenye baraza hilo kwa ajili
ya maamuzi baada ya baraza kujigeuza kama kamati na kujadili na hatimaye kutoka
na maamuzi Ikiwemo kufukuzwa kazi
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio
Mtawa ndiye aliyetoa taarifa ya maamuzi hayo mbele ya baraza
Akitilia mkazo maamuzi hayo mwenyekiti wa halmashauri Mh
Mtawa amesema wamepitia kwa makini mashauri hayo ya kinidhamu kuhakikisha haki
inatendeka kwa kila mtumishi huku akiwahakikishia kuwa watumishi wote wa
halmashauri wapo kwenye mikono salama katika baraza la madiwani linalotenda
haki kwa kila mmoja
Sikiliza sauti hii ya dakika 19 ikielezea kila kitu