Tajiri aliyenunua Nyumba za Lugumi apelekwa polisi

Mtu aliyetambulika kwa jina la Dk Louis Shika aliyenunua nyumba za Lugumi ambazo zimepigwa mnada na kampuni ya udalali ya Yono hii leo, amepelekwa kituo cha polisi kwa kukiuka masharti ya ununuzi

Akiongea na mwandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yono Bi. Scolastica Kevela amesema tukio hilo limetokea wakati mnada ukiendelea, na alipotakiwa kutoa kiasi cha pesa kutanguliza malipo, hakukutwa na pesa akisema zinatoka Kenya.
"Ni kweli tumempeleka kituo cha polisi cha Surrender, aliambiwa atoe ile asilimia 25 ya mwanzo kama ambavyo sheria ilivyo akawa hana akisema hela inatoka Kenya, wakati masharti hayasemi hivyo na tulimtangazia kabla ya mnada, inaonekana hakujiandaa tukaamua tumpeleke polisi", amesema Bi. Scolastica Kevela
Kutokana na tukio hilo mnada wa nyumba hizo umelazimika kurudiwa upya ili kuweza kupata mnunuzi halali wa mali za Lugumi, ambazo serikali imeagiza zipigwe mnada kufidia deni wanalodaiwa na TRA.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo