RC Wangabo ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya shule ya sekondari Kirando, Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara wa shule hiyo pamoja na na kuongea na wanafunzi, taarifa iliyobainisha kupatikana kwa mimba saba kwa kipindi cha Januari hadi oktoba mwaka huu na kesi zote zipo polisi.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na matokea yake watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze kuwajibishwa na hatimae kupunguza kasi hiyo ya mimba kwa wananfunzi.
“Mwalimu Mkuu unapogundua tu kwamba mwananfunzi ana mimba mweke pembeni ita wazazi wake, washirikishe polisi wawachukue wawekwe ndani kwa muda wa saa 48, hadi hapo watakapomtaja muhusika wa mimba hiyo, ukifanya hivyo mara kadhaa mabadiliko yatatokea,” amesema Wangabo.
Aidha mkuu huyo wa mkoa ametahadharisha kuwa shule yeyote atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo, ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.
