Mmiliki wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Scolastica iliyopo mji wa Himo wilayani Moshi, Edward Shayo amefikishwa mahakamani leo Jumatatu kusomewa shitaka la mauaji.
Mmiliki huyo, pamoja na watu wengine wawili wamesomewa shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo, Huphrey Makundi (16) aliyekuwa kidato cha pili.
Shayo ametolewa hospitali ya rufaa ya KCMC alikolazwa na kupelekwa moja kwa moja Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Amesomewa shtaka hilo pamoja na mlinzi wa shule na mwalimu mmoja
Mtoto huyo alitoweka shuleni Novemba 11 na baadaye kubainika ameuawa baada ya maiti yake iliyozikwa kama ya mtu asiyefahamika, kufukuliwa Novemba 17.