Mtu mmoja Raia wa marekani (30) amefariki Dunia baada ya kuzama baharini alipokua akiogelea huko Nungwi ndani ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Kwamujibu wa taarifa zilizopatikana kwa waliokuepo karibu na tukio hilo na kuthibitishwa na kaimu Kamanda wa Polisi ambae pia ni Mkuu wa upelelezi mkoa wa Kaskazini Unguja Suleiman Hassan amesema tukio hilo limetokea saa sita na nusu Mchana hapo jana wakati marehemu huyo alikuwa anashuhulika katiaka harakati zake za kuogelea.
Amefahamisha kuwa kabla ya kifo chake marehemu alifika katika Hoteli ya Paradise huko Nugwi akiwa katika shuhuli za kuogelea ndipo alipozidiwa na maji nakufariki dunia hapo hapo.
Kaimu Kamanda ameendelea kutoa wito kwa wamiliki wa hoteli waweke watu karibu na maeneo hayo ambapo likitokezea tatizo kama hilo iwe nirahisi kuwahi mapema kabla tatizokubwa kutokezea.